January 13, 2020


ADAM Salamba, mtanzania anayekipiga kwa sasa ndani ya timu ya Al-Jahra SC, iliyopo Uarabuni amesema kuwa ushirikiano anaopewa na wachezaji wenzake ni mkubwa.

Akizungumza na Saleh Jembe, Salamba amesema kuwa amekuwa akifurahia maisha ya huko kutokana na ushirikiano anaopewa na wachezaji wenzake.

"Huku ninaishi vizuri na wenzangu, tunashirkiana vema na kila mchezaji jambo ambalo linanifanya niwe na furaha.

"Nafanya yote kutokana na kupenda kazi yangu, nipo huku ila napeperusha vema bendera ya Tanzania kwani wengi wanapenda kutambua habari za nyumbani," amesema Salamba.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic