Klabu ya soka ya JKT Tanzania ipo mbioni kunasa saini ya beki wa kushoto ili kuziba nafasi iliyoachwa na mchezaji Adeyum Ahmad Suleiman aliyetimkia Yanga.
Klabu hiyo ambayo hivi karibuni imefanikiwa kuwarudisha wachezaji wake wawili waliokuwa wakicheza kwa mkopo katika Klabu ya Green Warriors na kumpandisha kinda kutoka kikosi B, Kevin Nashon.
Kocha wa JKT, Abdallah Mohamed, alisema: “Mpaka sasa tumefanikiwa kuwarudisha wachezaji wetu wawili kutoka Klabu ya Green Warriors ambao ni Majaliwa Shabani na Edson Katanga lakini pia tumemwongeza kinda Kevin Nashon na tuna mpango wa kumsajili beki mmoja wa kushoto ili kuziba pengo la Adeyum Suleiman na mpaka hivi sasa tuko kwenye mazungumzo na baadhi ya wachezaji.”
Klabu ya soka ya JKT ipo katika nafasi ya tisa katika msimamo wa ligi kuu ikiwa imeshacheza michezo 15, ikishinda michezo sita, imetoka sare michezo minne na kupoteza michezo mitano.
0 COMMENTS:
Post a Comment