BEKI wa Brighton, Ben White imeripotiwa kuwa ameziingiza vitani timu kubwa zinazoshiriki Ligi Kuu England ikiwa ni pamoja na Liverpool, Chelsea na Tottenham ambazo zinahitaji saini yake.
Beki huyo kwa sasa anakipiga kwa mkopo kwenye timu ya Leeds ambayo yupo kwa sasa na jana alianza kwenye kikosi kilichochapwa bao 1-0 mbele ya Arsenal kwenye mechi ya FA lililofungwa na Reiss Nelson dakika ya 55.
Beki huyo mwenye umri wa miaka 22 amekuwa kwenye ubora wake baada ya kujiunga na Leeds jambo ambalo limewavutia mabosi wa timu nyingi.
0 COMMENTS:
Post a Comment