MBELGIJI wa Yanga, LUC Eymaela ameanza leo kuwapeleka kwa kasi wachezaji wake wa Yanga kwenye mazoezi yaliyofanyika Uwanja wa Polisi.
Eymaela ameanza kukinoa kikosi hicho ambacho kinajiandaa na mchezo wake dhidi ya Kagera Sugar utakaochezwa Jumatano, Uwanja wa Taifa.
Eymaela amekuja Bongo kuchukua nafasi ya Mwinyi Zahera ambaye alipigwa chini ndani ya Yanga na nafasi yake ilikuwa inasimamiwa na Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga Charlse Mkwasa.
Yanga ipo nafasi ya saba ina pointi 25 ikiwa imecheza mechi 12 na Kagera Sugar ipo nafasi ya nane ikiwa imecheza mechi 16 na ina pointi 24.
0 COMMENTS:
Post a Comment