January 13, 2020



TIMU ya mpira wa kikapu ya Benki ya NMB imeibuka na ushindi wa vikapu 68 dhidi ya 52 vya timu ya Baraza la Wawakilishi.

Mchezo huo wa kirafiki ulikuwa maalumu kwa ajili ya maadhamisho ya miaka 56 ya Zanzibar na ulifanyika Visiwani Zanzibar kwenye Viwanja vya Mao Zedong na washindi walikabidhiwa kombe maalumu na medali.



Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Zuber Ali Maulid aliwakabidhi Kombe maalumu washindi hao ambapo alimpatia kapteni wa timu Danford Kisinda. Kwa upande wa timu za mpira wa miguu timu ya Shaurimoyo ilishinda kwa mikwaju ya penalti 5-4 dhidi ya timu ya Benki ya NMB baada ya dakika tisini kukamilika kwa sare ya bila kufungana.
  



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic