January 1, 2020


GERSON Fraga, kiungo mkabaji wa timu ya Simba, raia wa Brazil amefunga bao lake la kwanza ndani ya Ligi Kuu Bara baada ya kupita dakika 630 ambazo amezicheza akiwa na Simba msimu huu kabla ya mchezo wa jana dhidi ya Ndanda uwanja wa Taifa.
Fraga akiwa ndani ya Simba, wakati ikiwa chini ya Patrcik Aussems ambaye kwa sasa amepigwa chini kutokana na kile kilichoelezwa ni utovu wa nidhamu pamoja na matokeo mabovu alicheza jumla ya mechi sita bila kufunga amepachika bao lake la kwanza chini ya kocha Sven Vanderbroek aliyeongoza mechi mbili za ligi kwani kwenye mchezo dhidi ya Lipuli aliwekwa benchi.
Mpaka sasa Simba imecheza jumla ya mechi 12 ambazo ni sawa na dakika 1,080 na ina pointi 31 imefunga jumla ya mabao 27 na katika mabao hayo Fraga analo bao moja alilofunga mbele ya KMC akiwa nje ya 18 akimalizia pasi ya Francis Kahata.
Mechi ambazo Fraga alizecha ni dhidi ya JKT Tanzania, Simba ilishinda mabao 3-1, Simba 2-1 Mtibwa Sugar, Kagera Sugar 0-3 Simba, Simba 1-0 Azam FC, Mwadui 1-0 Simba, Ruvu Shooting 0-3 Simba, Simba 2-0 KMC alifunga bao dakika ya 90.
Alikaa benchi dhidi ya Biashara United Simba ilishinda mabao 2-0,Singida United 0-1 Simba,Simba 4-0 Mbeya City, Simba 4-0 Lipuli.Kwenye mchezo dhidi ya Tanzania Prisons uliochezwa uwanja wa Uhuru Fraga alikosekana hadi benchi.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic