January 17, 2020

IMEELEZWA kuwa Yanga imezipeperusha milioni 250 ndani ya dakika 180 ambazo ni sawa na mechi mbili walizocheza wachezaji wao kwenye mechi za Ligi Kuu Bara ndani ya mwaka mpya 2020.

Yanga iliyochini ya Kocha Mkuu, Luc Eymael raia wa Ubelgiji aliyeletwa na mabosi wa GSM iliahidiwa milioni 10 mezani endapo angeshinda mbele ya Kagera Sugar mwisho wa siku iliambulia kichapo cha mabao 3-0 kikaziotesha mbawa milioni 10 zikapeperuka jumla.

Habari kutoka ndani ya Yanga zinaeleza kuwa mechi ya kwanza iliyochezwa Januari 4 mwaka huu, 2020 mbele ya Simba iliotesha mbawa milioni 150 kutokana na Yanga kushindwa kuitungua mabao Simba.

"Kwenye mechi dhidi ya Simba wakati timu inapata sare ya mabao 2-2, mezani kulikuwa na milioni 200 za GSM, Ila ile sare iliokoa milioni 50 tu, sasa hapo ukijumlisha na zile 10 za Kagera zilizopeperuka jumla inakuwa milioni 250, sio mkwanja mdogo unauma kinoma," alieleza mtoa taarifa.

Eymael baada ya mchezo alisema kuwa walistahili kushinda ila wachezaji wake hawakuwa makini kutumia nafasi walizotengeneza atatumia makosa hayo kuwarekebisha kabla ya kuwavaa Azam FC, Kesho Uwanja wa Taifa.

4 COMMENTS:

  1. Duh! ofisi nzima hakuna hata anayejua hesabu za kumjumlisha na kutoa!

    ReplyDelete
  2. unajua mimi husoma habari zenu wakati mwingine nashindwa kuelewa uwezo wenu kufikiria..ila leo kushinda kwako kukokotoa hiyo hesabu nimetambua uwezo wako...endelea tu kuandika upuuzi

    ReplyDelete
  3. Saleh Jembe unaharibu kazi yako hata kama sio wewe vijana wako wanazingua taarifa zenu nyingi zina shida mi mtu ambae naingia kwenye hii account zaidi ya mara tano per day sijawahi kukosoa hila leo nimechoka jitahidi mzee plz

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic