BEKI kisiki wa Simba, Pascal Wawa amesema kuwa hawatailazia damu mechi yao dhidi ya Alliance, inayotarajiwa kuchezwa Januari, 20, Uwanja wa CCM Kirumba.
Simba jana ilikomba pointi tatu mbele ya Mbao kwa ushindi wa mabao 2-1 imebakiza dakika 90 kati ya 189 itakazotumia kanda ya ziwa.
Akizungumza na Saleh Jembe, Wawa amesema kuwa wachezaji wote wamekubaliana kusahau maumivu ya kulikosa taji la Mapinduzi na badala yake waongeze nguvu kwenye mechi za ligi.
"Kuhusu Mapinduzi haikuwa bahati yetu tumeumia kulikosa kombe Ila hatuna namna kwa sasa nguvu zetu ni kwenye mechi za ligi, tutapambana mbele ya Alliance kuibuka na pointi tatu muhimu, mashabiki wajitokeze kutupa sapoti," amesema Wawa.
Msimu wa 2018/19 Simba iliichapa nje ndani Alliance kwa jumla ya mabao 7-1, mechi ya Kwanza iliyochezwa Taifa, Simba ilishinda mabao 5-1 na ule wa pili ilishinda mabao 2-0.
Tunaomba muweke kikosi cha maana plz.
ReplyDeleteThis comment has been removed by the author.
ReplyDelete