January 8, 2020


Charles Boniface Mkwasa, Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga, amesema kuwa kilichowaponza Simba kushindwa kulinda mabao yao mawili waliyofunga Jumamosi iliyopita katika Uwanja wa Taifa, ni uvivu wa wachezaji wake kiujumla.

Simba iliwakaribisha Yanga kwenye mechi iliyosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wao ila waliambulia sare ya kufungana mabao 2-2, licha ya Simba kuanza kufunga mabao yote mawili.

Mkwasa alisema kuwa alitambua udhaifu wa wachezaji wa Simba ni uvivu na kutokuwa na uwezo wa kuhimili mikikimikiki kwa dakika 90, jambo lililofanya awabane mbavu kipindi cha pili.

“Ukiachana na aina ya timu niliyokuwa nacheza nayo kutegemea penalti pia wachezaji wake ni wavivu kwenye suala la ubora wao na utimamu jambo ambalo lilinifanya nikabadili mbinu kipindi cha pili, nilijua kwamba lazima watachoka na watashindwa kwenda na kasi ambayo nitawapeleka.

“Nilishindwa kwenda nao kipindi cha kwanza kwa kasi yao ili kuwasoma. Kulikuwa na uwezekano wa kuwafunga kabisa, bahati muda haukutosha,” alisema Mkwasa.

7 COMMENTS:

  1. Asante bro. Sasa hivi kila neno litasemwa maana tulikosea sisi kuruhusu sare. Muhimu Yanga wasijisahau madhaifu yao kwa hiyo droo wakadhani wanatimu nzuri au Mkwasa anambinu kama Klop.

    ReplyDelete
  2. Wavivu wachezaji wa Simba ni kweli kabisa kwani baada ya Muzamiru kupoteza mpira hakufanya jitihada zozote za kumkaba mapinduzi balama. Kweli chungu mimi Simba Damu ila asante Mkwasa kwa kupasua jipu huo ndio uzalendo .

    ReplyDelete
  3. Ndanda walishangilia kufungwa bao mbili!Kinachoendelea na ambacho ni bayana kabisa ni ushangiliaji wa sare!Mnachotuonyesha ni thamani yenu.
    Imekuwa kama mtoto wa maskini akipewa chupa ya Soda basi atainywa pole pole hadi hataa masaa sita atailuta bado.Ndugu mwandishi hii habari ya Mkwasa aliishaiongelewa katika blog..Hebu rudi kwenye tareh 5 Jan habari la Tamko la Yanga kuhusiana na penalti..
    Kuendelea kushangilia sare inaonyesha thamani yenu..Huko visiwani isitokee timu ikaikwepa Nyingine...tukutane fainali

    ReplyDelete
  4. Nammi natakata tukutane fainalii simbaa huna hatari yoyote ww unawachezaji wazeee kwanzaa

    ReplyDelete
  5. Master acha kuwaongelea hao mikia fc,kitendo cha kutaja mapungufu yao ni sawa na kuwapa mbinu,we piga kazi tu usiwe km Zahera.

    ReplyDelete
  6. Tuombe duwa tukutane nao Katika fainali zakombe la mapinduzi. Kilichowaharibikia Simba ni pale walipowadharau Yanga baada ya kuwachapa bao mbili lakini wasitaraji hayo tena

    ReplyDelete
  7. Da kwa kweli hata nchi zingne ligi zao ziko hvi kutoka tarehe nne mpaka sasa bado n habari za mkwasa na Yanga duuuuu. jamani hapo ni sale sipati picha kama Yanga wangeshnda kwanni mbona simba ni timu za ligi kuu Tz bara nbona mpaka kero na kuna habari nyingi sana za kuandika katika nyanja hii ya michezo. INACHOSHAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA INAKERAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic