January 12, 2020


LUC Eymael, Kocha Mkuu mpya wa Yanga ambaye yupo Bongo kwa sasa akikamilisha taratibu za awali ameyataka majina ya wachezaji wanne wa Yanga ili atazame maendeleo yao.

Eymael ambaye ni raia wa Ubelgiji alitua nchini Januari, 9 na kuunganisha moja kwa moja Visiwan Zanzibara ambapo timu ya Yanga ilikuwa inacheza mchezo wa nusu fainali dhidi ya Mtibwa Sugar na alishuhudia ikilazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na kutolewa kwa changamoto ya penalti 4-2.

Habari kutoka ndani ya Yanga zinaeleza kuwa alipokuwa uwanjani alimtazama namna mlinda mlango namba tatu Ramadhan Kabwili alichokuwa anakifanya pamoja na pasi mpenyezo za Mapinduzi Balama.

"Kocha alitazama mchezo kitofauti kwani alikuwa anaandka majina na mfumo ambao anaona utawafaa wachezaji wa Yanga kwa ajili ya kuleta ushindani kwenye mechi zingine.

"Miongoni mwa wachezaji ambao amewaulizia ni Kabwili, Balama, Deus Kaseke pia alikuwa anaulizia kuhusu Yondani ambaye hakucheza muda mrefu kwa kutumia nguvu ila aliona kitu," alieleza mtoa taarifa huyo.

Eymael amesema kuwa amewatazama baadhi ya wachezaji na ameshapata picha ya namna kikosi kilivyo kwani wachezaji huwa tofauti ila mfumo ndio ambao unawabeba ndani ya timu hivyo atawajengea uwezo wa kujiamini na kucheza kwa mbinu zote.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic