AWADH salum, mshambuliaji wa Mtibwa Sugar amesema kuwa walijipanga kupata ushindi mbele ya Mbao FC kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu Bara uliochezwa jana uwanja wa CCM Gairo, Morogoro.
Kwenye mchezo huo ambao mchezaji bora wa mwezi Oktoba, Jaffary Kibaya alikabidhiwa tuzo yake ya mchezaji bora alitoa pasi ya bao dakika ya 70 lililopachikwa na Salum.
"Tulijipanga kufanya vizuri, tulijituma uwanjani na matokeo yetu yanatokana na kufuata maelekezo ya mwalimu wetu hivvyo tu hakuna jambo jingine, " amesema.
Matokeo hayo yanaifanya Mtibwa Sugar kusepa na pointi tau na kufikisha jumla ya pointi 22 ikiwa nafasi ya 7 baada ya kucheza mechi 15 huku Mbao FC ikiwa nafasi ya 14 na pointi zake 17 baada ya kucheza mechi 15.
0 COMMENTS:
Post a Comment