UONGOZI wa KMC umesema kuwa umejipanga ndani ya mwaka 2020 kutafanya mambo makubwa yatakayourejesha kwenye ubora wake.
KMC iliyo chini ya Kaimu Kocha, Ahmed Ally ilifunga mwaka 2019 kwa kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Mwadui FC, mchezo uliochezwa Desemba 31, uwanja wa Kambarage, Shinyanga.
Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa KMC, Anwar Binde amesema kuwa makosa waliyoyafanya mwaka 2019 wameyatambua na wanayafanyia kazi.
"Tunajua kwamba hatukuanza vizuri ila haimaanishi kwamba hatuwezi kurejea kwenye ubora wetu kila kitu kinawekezkana.
"Mpango mkubwa ndani ya mwaka 2020 kuwa bora na kupata matokeo chanya, mashabiki watupe sapoti na waendelee kuwa pamoja nasi kwani tunaweza," amesema.
KMC kesho itashuka uwanja wa Sheikh Amri Abeid kumenyana na Singida United iliyo nafasi ya 20 na pointi zake 7.
0 COMMENTS:
Post a Comment