UONGOZI wa Mtibwa Sugar umesema kuwa hauna mashaka na mchezo wao wa leo dhidi ya Yanga wa nusu fainali Kombe la Mapinduzi utakaochezwa Uwanja wa Amaan kwani wapo tayari kuibuka na ushindi na kombe ndio malengo yao.
Mtibwa Sugar ilitinga hatua hiyo kwa ushindi wa penalti 4-1 mbele ya Chipukizi baada ya sare ya kufungana bao 1-1 ndani ya dakika tisini kwenye mchezo wao uliochezwa uwanja wa Amaan.
Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema kuwa wamejipanga kufanya vizuri kwenye mchezo wao bila kujali watacheza na nani.
“Mtibwa Sugar siku zote tupo vizuri kwani falsafa yetu ipo makini na hatutishwi na wapinzani wetu Yanga, tunahitaji kupata matokeo chanya yatakayotupeleka hatua ya fainali ambapo tutatimiza lengo letu la kutwaa kombe.
“Timu zote ni nzuri na tunaziheshimu ndio maana zipo kweye ushindani ila kwetu sisi tunaamini anina ya wachezaji tulionao utaongea kwa vitendo uwanjani, mashabiki watupe sapoti,” amesema Kifaru.
Mchezo huu utachezwa leo saa 2:15 Usiku na utarushwa moja kwa moja kupitia Azam TV.
0 COMMENTS:
Post a Comment