January 2, 2020




Uongozi wa Simba umekubali kibali cha kazi cha Haruna Niyonzima kitumike akiwa kazini Yanga.

Kumekuwa na utata kuhusiana na suala la Niyonzima ambaye amerejea Yanga atafanya vipi kazi.

Simba ilimkatia kibali hicho cha miaka miwili, akakitumia kwa mwaka mmoja kabla ya kuondoka nchini na kurejea kwao Rwanda.

Aliporejea nchini leo, kawaida hawezi kupata kibali kipya hadi kile kilichopo kiishe na Simba ndio walikuwa na kibali hicho.

"Hivyo Simba ni lazima watoe kile kibali, haviwezi kutolewa vibali viwili kwa wakati mmoja, kilieleza chanzo," alisema.

Yanga walipiga katika ofisi za Simba leo na kufanya mazungumzo kuhusiana na hilo na taarifa zimeelezwa kuwa wamekubaliana.

"Tumekubaliana, tutawapa kibali ili wamtumie mchezaji wao," kilieleza chanzo kingine kutoka Simba.


Niyonzima ameungana na Yanga katika mazoezi ya mwishomwisho kabla ya kuivaa Simba kwenye UWanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, keshokutwa.


Niyonzima anareja Yanga kwa mara ya pili akitokea AS Kigali, kabla alijiunga na Yanga akitokea APR ya Rwanda.

4 COMMENTS:

  1. Gongo wazi wasingekubali. Uungwana mkubwa sana kutoka kwa Simba.

    ReplyDelete
  2. This is simba brother,wasijefungwa wakapata kisingizio acha wachezeshe ikiwezekana waombe waingie 22 badala ya 11 ha ha ha ha ha .

    ReplyDelete
  3. Simba imefanya uungwana mkubwa wa kupigiwa mfano na iwe mfano kwa wote

    ReplyDelete
  4. Soka ni burudani sio uadui,heko Simba kweli nyie ni level nyingine

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic