ZUBER Katwila, Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar amesema kuwa wachezaji wake wote wana deni kutokana na kusema kuwa mechi ya Yanga ilikuwa ngumu kuliko ya leo dhidi ya Simba.
Yanga ilitolewa na Mtibwa Sugar kwenye mechi ya nusu fainali na Mtibwa Sugar kwa penalti 4-2 baada ya dakika tisini kutoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1.
Katwila amesema kuwa ameskia baadhi ya wachezaji wakisema hivyo jambo linalowafanya wawe na deni la kulipa kwenye mechi ya leo dhid ya Simba.
"Kauli za mchezaji mmojammoja ambazo zimetolewa ni deni kwao kwani kwa sasa wanatakiwa waziunganishe kauli hizo na kuzifanya ziwe na umoja katika yale ambayo wameyasema na kuonyesha vitendo.
"Wachezaji wanatakiwa waonyeshe kwa vitendo kile ambacho wamewaaminisha mashabiki wao kwani mpira wa miguu sio maneno bali ni vitendo,nina amini utakuwa mchezo mgumu nasi tutapambana kufanya vizuri," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment