January 3, 2020


SALEH Ally, 'Jembe' mmiliki wa blog ya michezo ya Saleh Jembe ameipongeza kampuni ya Star Media kupitia brand yake ya  StarTimes, kwa kupata kibali cha kuonyesha michuano ya Kombe la FA (Emirates FA Cup).



Jembe amesema hayo wakati wa uzinduzi wa uonyeshwaji wa mechi hizo yeye alipochambua kwa kushirikiana na mchambuzi mwingine mahiri, Shaffi Dauda na wengine kuhusiana na michuano hiyo na mechi zake.

StarTimes itaanza kuonyesha ufunguzi wake kwa maana ya mchezo wa Ngao ya Jamii (FA Community Shield) na watakuwa wakirusha matangazo ya mechi zote mubashara kutoka nchini Uingereza.


Jembe amesema kuwa ni hatua kubwa na inapaswa kupongezwa kwa kampuni hiyo kuendelea kupiga hatua kila iitwapo leo kwenye masuala ya michezo na ubora wa kile ambacho wanakifanya.


"2020 imeanza kipekee na ninapenda kuipongeza kampuni ya Star Media kupitia brand yake ya StarTimes kuweza kuonyesha michuano ya Kombe la FA (Emirates Cup).


"Ninaamini itatoa fursa kwa wapenda michezo dunaini kote kushuhudia burudani mojakwamoja hasa baada ya kupata kibali, wengi wanapenda soka na kwa sasa ushindani umekuwa mkubwa huku kampuni ya Star Media ikizidi kuwa bora siku zote, kwa hili wanastahili pongezi," amesema.



StarTimes imepata rasmi kibali hicho ambacho itakuwa ni mahususi kwa kurusha michezo hiyo katika nchi zote za kusini mwa  jangwa la Sahara kupitia lugha mbalimbali kibali ambacho kitadumu mpaka mwishoni mwa mwaka 2021.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic