BEKI ya NMB imewapiga tafu wana michezo wa Visiwani Zanzibar kwa kutoa vifaa vya michezo kwa ajili ya kusherehekea miaka 56 ya Mapinduzi.
Zoezi hilo la kukabidhi vifaa hivyo limefanywa na Meneja wa
NMB tawi la Zanzibar, Abdallah Duchi ambaye alimkabidhi vifaa vya michezo Salim Ali
Jazira kwa ajili ya timu ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Vifaa hivyo ni pamoja na Jezi na Mipira kwa ajili ya michezo
ya kusherehekea miaka 56 ya mapinduzi ya Zanzibar.
Thamani ya vifaa hivyo ambavyo ni kwa ajili ya Mpira wa Miguu na Kikapu vyote ni shilingi milioni 6.5. Hafla ya makabidhiano
ilifanyika kwenye ukumbi mdogo wa Baraza la Wawakilishi Chukwani Zanzibar jana.
0 COMMENTS:
Post a Comment