January 10, 2020

UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa utapambana leo mbele ya Simba ili kutinga hatua ya fainali ya Kombe la Mapinduzi.

Azam FC itacheza leo saa 2:15 usiku mchezo utakaochezwa Uwanja wa Amaan.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffary Maganga amesema kuwa kikosi kimefanya mazoezi na kipo kwenye morali kubwa.

"Sisi ni mabingwa watetezi hilo lipo wazi, tunawaheshimu Simba na tutapambana kupata matokeo mazuri, sapoti ya mashabiki tunahitaji," amesema.

Azam FC ilitinga hatua ya nusu fainali kwa kuitwanga Mlandege bao 1-0 lililopachikwa na Obrey Chirwa na Simba ilipenya hatua hiyo kwa ushindi wa mabao 3-1 mbele ya Zimamoto.

Mshindi wa mchezo wa leo atamenyana na mshindi wa kwanza ambaye ni Mtibwa Sugar aliyemtoa Yanga kwa mikwaju ya penalti 4-2 mchezo uliochezwa jana, Januari 9. 

1 COMMENTS:

  1. Masikini Yanga inasikitisha Sana. Kati ya mikakati yetu Ilikuwa tuchukue makombe yote lakini tunavoona sasa ni mwendo wa kuchechemea na huku baadhi ya nyota wakizidi kujitenga au kuten gwa na huku baadhi ya viongozi Kufukuta chini kwa chini na kwa watani poa kwa kila upande

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic