January 10, 2020


Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu amesema kuwa kwa sasa hawako tayari kuzungumzia juu ya uwezekano wa kukutana na Yanga katika fainali kabla ya mchezo wa nusu fainali.

Ameyasema hayo katika mkutano na wanahabari kisiwani Ugunja kuelekea mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi dhidi ya Azam FC utakaopigwa kesho Januari 10.

Rweyemamu amesema kuwa kuizungumzia Yanga hivi sasa itakuwa ni kutoitendea haki game hii ya sasa ya nusu fainali iliyo mbele yao.

"Kwa bahati tumepata timu bora kwenye nusu fainali hii, kwa maana ya Simba, Yanga, Azam FC na Mtibwa Sugar. Fainali itakuwa nzuri kwa timu yoyote itakayovuka na sisi akili yetu yote tunaelekeza kwenye mchezo huu na baada ya hapo tutaizungumzia fainali dhidi ya Yanga", amesema Rweyemamu.

Kwa upande wa Azam FC ikiongozwa na Meneja wake Philip Alando, umesema kuwa wamejiandaa kwa ajili ya mchezo huo na mazoezi yao yako vizuri kuelekea mchezo.

Yanga inacheza na Mtibwa Sugar leo katika nusu fainali ya kwanza huku Simba ikitarajia kupambana na Azam FC hapo kesho na mchezo wa fainali ukitarajia kupigwa Januari 12.

CHANZO: EATV

14 COMMENTS:

  1. Wengi wenye tabia yakwenda uwanjani na matokeo mnazidi kuumbuka,mpira hauna mwenyewe jamani eti mlikua mmeshapanga timu zitakazo cheza fainali hatimae wamecheza mpira wa kihanisi,jifunzeni kitu hapa kubalini madhaifu yenu yanga mlijiamin kupita kiasi hatimae mmetolewa.

    ReplyDelete
  2. Mnakuja kujitetea kwa points dhaifu eti hatukutaka wachezaji wetu waumie tumewahifadhi kwa ajili ya ligi kuu,kweli inaingia akilin hiyo dah NUGAZ acha unazi brother yule sio kocha na kama huamin utakuja kutupa mrejesho muda sio mrefu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kuna uhusiano wowote wa Yanga kufungwa mapinduzi jana na kocha mpya aliyeajiriwa? We umrmtathmini na umempima lini mpaka ukakomenti kuwa siyo kocha mzuri? Haya tuambie kocha mzuri yuko wapi na una tumia vigezo gani kumwona mzuri au si mzuri?

      Delete
    2. KANISHANGAZA SANA HUYO SHABIKI MAANDAZI.....ANAONGEA VITU AMBAVYO HAVIELEWI,ANACHANGANYA MADA.

      Delete
    3. Mpira hamjui mnakurupuka tu kwani mliambiwa teams ni Simba na Yanga tu enzi hizo kuna pan africa cda mecco ushirika kimanumanu hata wajinga kama hawa waropokaji hawakuwepo Coach kaja kuangalia team wala hajaanza kazi wewe wajambaa tuu. Yaani Simba icheze vimechi viwili ije kukutana na Yanga ili iweje ndio itacheza club bingwa??? mashindano ya kisiasa mnataka kutuharibia mpira focus yetu iko kwenye league na TUNAKUJA narudia TUNAKUJA KUKAAA KILELENI MPAKA LIGI IISHE

      Delete
  3. kweli walipumzisha kikosi cha maana ili kicheze fainali...lakini pia inawezekana waliikwepa Simba fainali...kocha ni mbovu sana kila alikotoka hakuwa kwenye 10 bora

    ReplyDelete
  4. Tunatoa hongera kwa Yanga kwa kunusurika kurejea kinywani mwa Simba na waishukuru Mtibwa ikiwa ni muokozi

    ReplyDelete
  5. Bahati mbaya sjawahi kumsikia nugaz akiongea point sasa sjajua i makusudia au anajua mashabiki wa yanga walivyo kwa hyo inamlazimu kuwafanania? ngoja nimfuatilie kwenye mambo mengine nje na mpira nitakuja na majibu hapa

    ReplyDelete
  6. Mr unknown at 7:57 ungefanya hivyo hata mimi ningekuunga mkono huyu jamaa hakuna kitu kwakweli,anaongeaga ujinga tu sasa angalia baada ya kutolewa mapinduzi alivyokua anaongea pumba tena zilizochacha,jamaa hovyo sana ila bado lazima wafe round ya pili.

    ReplyDelete
  7. mashindano madogo madogo yasituumizie wachezaji yaheee!Wakiingia uwanjani ni kutumia nguvu na sio utaalaam...Jana Mtibwa katawala mchezo

    ReplyDelete
  8. Mashabiki eti mshaanzaa kumponda kocha kama yy ndio alopanga team kudadadadeki

    ReplyDelete
  9. Acheni upumbavu. Kocha mpya Yanga hapo anaingiaje kwenyr matokeo ya timu jana?

    ReplyDelete
  10. Amekuja na mkosi.Mechi ya kwanza kuangalia vyura wamepigwa.Eti Nugaz anadai ingesababisha wachezaji waumie???Naona jamaa make up inaathiri uwezo wa kuchanganua mambo.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hujui mpira inaonekana bado unakaa kwa baba yako hizo zinaitwa changamoto au challeges kwa kikatoliki ndio maana akaitwa mwalimu au kocha sasa aje team ishinde ili nini grow up kula kulala wewe DAIMA MBELE TUNAKUJA KAMA TULIVYOSEMA TUNATAKA KOMBE LETU

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic