UONGOZI wa Tottenham, umeonesha nia ya kuipata saini ya mshambuliaji wa AC Milan, Krzysztof Piatek.
Mpango wao wa kwanza uliokuwa kumpata nyota huyo kwa mkopo, inaelezwa kuwa umekataliwa jambo lililowafanya mabosi wa Tottenham kuvunja beki kuipata saini ya nyota huyo.
Nyota huyo pia alikuwa anahitajika kwa mkopo kwenye timu ya Newcastel United na Aston Villa ila mabosi wake wamekataa dili hilo wanahitaji pauni milioni 30 ili wamuache. .
Ujio wa Zlatan brahimovic umemtisha nyota huyo na anataka kuondoka ndani ya kikosi hicho.
Kuumia kwa mshambuliaji tegemeo wa Spurs Harry Kane kunamaanisha kwamba Spurs lazima wamtafute mbadala wake huku Piatek akipewa chapuo kubwa kwenye usajili wa mwezi Januari.
Kane anatarajiwa kurejea kwenye mafuzo mwezi Aprili kutokana na kusumbuliwa na majeruhi.
0 COMMENTS:
Post a Comment