January 1, 2020


INAELEZWA uongozi wa Simba umeamua kuongeza nguvu katika kitengo cha afya baada ya kumuongeza kimyakimya mtaalam wa viungo ‘fizisio’ aliyefahamika kwa jina la Jairon kwa ajili ya kusaidiana na aliyepo Paul Gomez, raia wa Ujerumani.

Haya yote yanafanyika zikiwa zimebaki siku chache kabla ya mchezo dhidi ya watani wao wa jadi, Yanga, Januari 4. Simba inapambana kuhakikisha inashinda mchezo huo.

Simba imemuongeza mtaalamu huyo kwa lengo la kusaidiana na Gomez ambaye inaelezwa kuwa ni miongoni mwa wanaotarajia kuondoka kama ilivyokuwa kwa kocha mkuu, Patrick Aussem na msaidizi wake Denis Kitambi, kufuatia uwepo wa madai ya rekodi mbaya kwenye kazi yake ya kuwatibu wachezaji wa timu hiyo.

Championi linafahamu kuwa mtaalam huyo ameanza kazi hivi karibuni licha ya uongozi kutomtambulisha rasmi lakini amekuwa akionekana akifanya mazoezi ya timu hiyo pamoja na kuwepo katika mechi mbili zilizopita katika Ligi Kuu Bara wakati wa mazoezi ya awali.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya timu hiyo, kimeeleza kuwa mtaalamu huyo ameanza kazi hiyo kwa lengo kusaidiana na Gomez ambaye huenda akaondoka wakati wowote ndani ya timu hiyo.

Championi lilimtafuta meneja wa timu hiyo, Patrick Rweyemamu ambaye alikiri kuwepo kwa mtaalamu huyo licha ya kutoweza kukaa benchi kutokana na idadi ya watu watano pekee ambao hutakiwa kukaa kwenye benchi mbali ya wachezaji.

“Ni kweli huyo mtu yupo, amekuja kama mtaalamu wa viungo na sasa anasaidiana kufanya kazi na Gomez, hawezi kukaa benchi isipokuwa anafanya mazoezini pamoja na kipindi cha mazoezi ya awali kabla ya mechi kwa kuwa idadi ya watu wanaokaa wakati wa mechi ni ndogo,” alisema Rweyemamu.

CHANZO: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic