January 1, 2020


Kuelekea Mtanange wa kukata na shoka mnamo Januari 4, 2020 kati ya watani wa jadi Simba na Yanga Kampuni  ya GSM Group ambao ni moja ya wadhamini wakuu wa timu ya Yanga kupitia Godoro la Chapa GSM inatarajia kutoa zawadi ya godoro la nchi 5x6x8 kwa mchezaji wa Yanga atakayeibuka nyota wa mchezo baina yao na Simba.

Pambano hilo la kukata na  shoka ambalo ni la kwanza msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara, litachezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Makao makuu ya Kampuni hiyo yaliyopo Mwenge jijini Dar es Salaam, Meneja Masoko na Mawasiliano wa GSM Group, Matina Nkurlu, alisema wameamua kutoa zawadi hiyo ili kuwapa morari wachezaji wa Yanga.

Alisema wao kama wadhamini wa Yanga ni wajibu wao kuhakikisha timu hiyo inawapa raha mashabiki wake kwa kushinda mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu na wapenzi wa soka hapa nchini na Afrika Mashariki kwa ujumla.

“Kuelekea mechi ya kukata na shoka kati ya watani wa jadi, Simba na Yanga, moja ya wadhamini wakuu wa timu ya Yanga, GSM Group kupitia godoro chapa GSM, tutatoa zawadi nono kwa mchezaji bora wa timu ya Yanga wakati wa mechi Yanga  na Simba kwa  kumzawadia godoro la nchi 5x6x8.

” Tunaamini zawadi hii itawaongezea wachezaji morali ya kupambana kuiwezesha Yanga kupata ushindi na hivyo kuwapa raha mashabiki wao na kuendelea kupata matokeo chanya kwa mechi zingine zijazo,” alisema Nkurlu.

Aliongeza: “Yanga ni klabu kubwa na bora hapa nchini kama ilivyo kwa magodoro yetu Chapa GSM hivyo mashabiki wao nao wanastahili matokeo yaliyo bora uwanjani ndio maana tumeamua kutoa zawadi ili kuwapandisha mzuka wachezaji wa Yanga kuelekea mchezo huo muhimu wa Jumamosi ya Januari 4.”

Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, aliishukuru GSM Group kwa ahadi hiyo ambayo anaamini itawaongezea hamasa wachezaji wa timu yao.

2 COMMENTS:

  1. Haya mazingira ya mitifuano na mfarakano si dalili nzuri kuelekea mechi ya Jumamosi...mashabiki wa Yanga wanavurugu kwa hiyo Nawaonea huruma Viongozi wa Yanga haya mambo yasije yakasababisha kutokea vurugu kubwa pindi timu itakapofungwa ....amani isije kutoweka si Jangwani tu bali nchi nzima....

    ReplyDelete
    Replies
    1. kati ya mashabiki ambao ni waelewa kabisa kuhusiana na matokeo ya uwanjani ni mashabiki wa yanga,wao huwa hawana shida eidha ya kutoka sare ama kufungwa na wala sina kumbukumbu kwamba kuna game ya simba na yanga ambapo yanga alifungwa na akafanya vurugu,ila kwa MIKIA FC wao kufanya vurugu pale wanapofungwa na yanga ni kawaida yao tu,na wakati mwingine hata wanapofungwa na tim ya kawaida kama KAGERA huwa hawaachi eidha kun'goa viti au kurusha chupa kwa waamuzi....kwa hio BRO Acha uchochezi...

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic