Kampuni ya Star Media kupitia brand yake ya StarTimes, imepata kibali
cha kuonyesha michuano ya Kombe la FA (Emirates FA Cup) ikianza na ufunguzi
wake kwa maana ya mchezo wa Ngao ya Jamii (FA Community Shield) ambapo watakuwa
wakirusha matangazo ya mechi zote mubashara kutoka nchini Uingereza.
Akitoa ufafanuzi wa kibali hicho Meneja Masoko wa kampuni hiyo, David
Malisa amesema,StarTimes imepata rasmi kibali hicho ambacho itakuwa ni mahususi
kwa kurusha michezo hiyo katika nchi zote za Kusini mwa Jangwa la Sahara kupitia lugha mbalimbali
kibali ambacho kitadumu mpaka mwishoni mwa mwaka 2021.
“Kwa niaba ya Mkurugezi wetu wa Idara ya Michezo kutoka makao makuu
yaliyopo Beijing China, Shi Maochu ametuambia kuwa, hii ni hatua kubwa kwa
michuano ya Emirates FA na Emirates Community Shield kurushwa kwetu, kwa sababu
yanajumuisha timu zote kubwa na bora
zilizopo nchini Uingereza, hivyo tunafuraha kubwa sana kuwa sehemu ya
kuonyesha michuano hiyo.
“Tunatambua wazi kuwa Watanzania wengi ni wapenzi wa mpira wa miguu,
hivyo kwa kutambua hilo na ndiyo maana nasi tumezingatia hili kwa kuwasogezea
matangazo yetu karibu ambapo watapata
burudani ikiwa ni sambamba na michuano ya kimataifa ya Copa Italia, na Bundesliga lakini
pia baadhi ya ligi za Ulaya kama UEFA
Europa League na Euro 2020.
Malisa aliongeza kwa kusema kuwa: “Pamoja na uwepo wa michuano mingi na
mikubwa kama hiyo, tutaendelea kuwaletea maudhui mbalimbali kwa gharama nafuu
kabisa hususani ndani ya mwaka huu wa 2020 ili tuweze kukidhi matarajio ya
watazamaji wetu kwani mashindano haya ya Kombe la Emirates FA 2019/2020
yataanza kurushwa rasmi Januari 4 mwaka
huu kwa maana ya kesho Jumamosi kupitia king’amuzi pendwa cha StarTimes.
“Lakini lazima watazamaji wetu wakumbuke kwamba matangazo haya yatakuwa mubashara kupitia chaneli 8 za michezo zilizopo kwenye king’amuzi chetu ila pia
tutarusha kupitia APP yetu ya StarTimes on live, hivyo unatakiwa kulipia mapema
king’amuzi chako kupitia bando la Uhuru
kwa shilingi 18000 tu hili kwa watumiaji wa Antenna na shilingi 21000 kwa
watumiaji wa Dish,” amesema Malisa.
0 COMMENTS:
Post a Comment