January 11, 2020


TAARIFA ya Tanzania kutoka kwa Uongozi wa Azam FC leo ipo namna hii:-

Azam FC tumepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha mke wa Nahodha wetu, Agrey Moris, aliyefariki dunia jana jioni wakati akiwa kwenye harakati za kujifungua.

Tunatoa salamu zetu za pole kwenda kwa familia ya Moris, pamoja na ndugu, jamaa na marafiki na wote walioguswa na msiba huo.

Azam FC tunaungana na familia ya marehemu na tunamuomba Mwenyezi Mungu, awajalie nguvu na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu.

Bwana ametoa na Bwana Ametwaa, Jina lake lihimidiwe. Amen.

4 COMMENTS:

  1. pole sana kaka Agrey.
    Mungu akupe wepesi katka wakati huu mgumu mno.
    Bwana alitoa na Bwana ametwaa Jina la Bwana lihimidiwe
    Aamina

    ReplyDelete
  2. Enter your comment...Agrey pole sana kwa msiba huu mzito. Tunamuomba Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema akutie nguvu wewe na familia katika kipindi kigumu cha msiba. Tusiongee mengi maana Mungu ndie muweza wa yote. BWANA AMETOA NA YEYE NDIE KATWAA. Jina lake lihimidiwe... Amina

    ReplyDelete
  3. Inna Lilah Wa Inna Kiayh Rajiun

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic