January 11, 2020


LENGENDARI wa timu ya Barcelona, Xavi Hernandez inaripotiwa kuwa amepewa dili la kuinoa timu hiyo kwa miaka miwili akichukua nafasi ya Ernesto Valverde ambaye atapigwa chini muda wowote kuanzia sasa.
Kiongozi wa Barcelona, Eric Abidal na Mtendaji Mkuu wa Barcelona Oscar Grau wametajwa kuhusika kufanya mazungumzo na nyota huyo wa zamani wa Barcelona mara baada ya kichapo cha mabao 3-2 walichopokea kutoka kwa Atletico Madrid kwenye mechi ya nusu fainali ya Kombe la Super Cup nchini Saudi Arabia.
Mkutano huo unaelezwa kuwa ulidumu kwa muda wa masaa mawili ulitosha kumshawishi bosi wa Barcelona kumpa dili hilo Xavi ili atue rasmi ndani ya Nou Camp.
Kutua kwa kocha huyo ndani ya timu hiyo kutampa wakati mgumu wa kuanza kuitengeneza timu upya ili iweze kutwaa taji la nane la La Liga pamoja na mashindano mengine atakayoshiriki . 
Pia wengine ambao wanatajwa kuhusika kutua Barcelona ni pamoja na Pep Guardiola anayeinoa Manchester City kwa sasa na Thiery Henry.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic