BAKARI Shime, Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania
ya Wanawake chini ya miaka U 17 amekiongoza kikosi chake kupata ushindi wa mabao
5-1 dhidi ya Burundi kwenye mchezo wa kuwania kufuzu tiketi ya kushiriki Kombe
la Dunia kwa Wanawake.
Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar, leo, Januari 12, ulishuhudiwa na mashabiki wengi waliojitokeza kuipa sapoti timu hiyo ambayo
imecheza soka la pasi nyingi na kushambulia.
Asha Masaka mshambuliaji wa U 17 alikuwa mwiba kwa
safu ya ulinzi ya Burundi na mlinda mlango wao, Amissa Inarukundo ambaye
aliokoteshwa nyavuni mabao matatu ya Asha aliyesepa na mpira wake huku Joyce Meshack na Protasia Mbunda
wakipachika bao mojamoja na kukamilisha jumla ya mabao matano kwa U 17 ya
Tanzania.
Bao pekee la kufuta machozi kwa Burundi lilipachikwa
na Nadine Ndayishimiye kutokana na uzembe wa safu ya ulinzi wa timu ya Taifa ya
Tanzania, U 17.
Michuano hiyo
inatarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu nchini India na mchezo wa marudio
unatarajiwa kufanyika Januari 25, nchini Burundi.
Shime amesema kuwa sapoti kubwa ya watanzania
imechangia kupata ushindi na vijana wamepambana kupata matokeo na malengo ni
kushiriki kombe la dunia kwa kuanza kuyafanyia kazi makosa waliyoyafanya Uwanja
wa Taifa.
Peace Olga nahodha wa Burundi amesema kuwa kilichowaponza ni ukubwa wa uwanja pamoja na nyasi bandia walizozizoea kwao tofauti na Taifa
0 COMMENTS:
Post a Comment