NAHODHA na kiungo wa Yanga, Mkongomani Papy Tshishimbi, amewachimba mkwara wapinzani wao Simba kwa kuwaambia wasitarajie kupata urahisi wakati ambao watakutana kutokana na wao kujipanga kufanya makubwa kwenye mechi hiyo.
Mkongomani huyo kwa mara ya kwanza ataiongoza Yanga kama nahodha wake mkuu wakati watakapopambana na wapinzani wao hao kwenye mechi hiyo ambayo itakuwa na ushindani mkubwa.
Kiungo huyo atawaongoza wenzake katika kutafuta nafasi ya kulipiza kisasi baada ya msimu uliopita katika mechi ya mwisho walipokutana kufungwa bao 1-0.
Tshishimbi amesema kwamba anaomba awepo kwenye mechi hiyo kwa ajili ya kuitetea klabu yake iweze kufanya vizuri na kupata matokeo mazuri katika mechi hiyo ambayo itakuwa na ushindani mkubwa.
“Ninachokiomba ni kuwa niwepo kwenye mechi hiyo kwa ajili ya kuisaidia timu yangu iweze kupata matokeo kama ambayo tunayahitaji.
“Tunajua ni mechi ngumu lakini tutapambana kwa ajili ya kuona tunakuwa bora na tunapata ushindi kwenye mechi hiyo kama ilivyo mechi nyingine,” alimaliza Mkongomani huyo.
Daima mbele nyuma mwiko!!!!
ReplyDeleteLazima vyura wakimbilie mbwani kwao mapema
ReplyDelete