January 1, 2020


Uongozi wa klabu ya Yanga umetangaza kuwa kiungo Haruna Niyonzima atawasili Jumatano ya wiki hii ambayo ni leo.

Kwa mujibu wa Ofisa Mhamasishaji wa timu hiyo, Antonio Nugaz, ameeleza kuwa mchezaji huyo anakamilisha taratibu kadhaa huko kwao Rwanda kwa ajili ya kuwasili Dar es Salaam.

Nugaz ameeleza na akiwataka wanayanga kutokuwa na wasiwasi juu ya mchezaji huyo kwani kuna masuala kadhaa ambayo anamalizia kuyakamilisha.

Yanga hivi sasa iko katika maandalizi ya mchezo dhidi ya watani wa jadi Simba ambayo itachezwa Januari 4 2020.

3 COMMENTS:

  1. Usumbufu ndio kawaida yake huyo. Bado akifika aanze kidengua hivi mnambembeleza kwa kiwango kipi? Wenye viwango kina Msuva si mnawaona wanazidi kwenda mbele? Usumbufu wa Niyonzima mmeutaka wenyewe

    ReplyDelete
  2. Yanga iwaweke wazi mashabiki wake ni kuwa As Kigali imegoma kumpa kibali Niyonzima hadi hapo itakapokamilishiwa ada ya uhamisho , waache kumtupia lawama kuwa anakamilisha masuala yake . Na pia uongozi uweke wazi sharti alilowapa kama umelitimiza kuwa alihitaji malipo yake yakafanyikie na kukamilikia Rwanda kabla hajasaini mkataba .Wasipotoa ufafanuzi wa hayo na tarehe 4 asiwe kikosi cha mchezo ambao kipigo kiko pale pale hata kama atakuwemo au asiwemo , Siku hiyo viongozi watafute mlango wa kutokea uwanjani

    ReplyDelete
    Replies
    1. unakurupuku kuongea usichokijua.......unaongea ki ushabiki maandazi zaidi......watu wa dizaini yako nimewafuatilia mara nyingi,hakuna mnachokijua ktk soka zaidi ya kupenda kubishana hata pale pasipostahili ubishi.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic