January 18, 2020


Nahodha na kiungo mkabaji wa Yanga, Mkongomani Papy Tshishimbi, huenda akakutana na msala kutoka kwa kocha mpya wa timu hiyo, Luc Eymael baada ya kupitiliza siku alizoomba za ruhusa katika timu hiyo.

Tshishimbi hajafanya mazoezi na Yanga tangu kocha huyo aanze kazi kikosini hapo wiki hii, kutokana na kile kilichoelezwa aliomba ruhusa ya kwenda kuitazama familia yake nchini DR Congo.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Spoti Xtra, kiungo huyo kabla ya kuruhusiwa kurudi kwao DR Congo, aliomba ruhusa ya siku tano kwa ajili ya kwenda kuiangalia familia yake wakati timu ilipokuwa inajiandaa kwenda Zanzibar kwenye Kombe la Mapinduzi.

“Kwa jinsi kocha huyu alivyokuwa mkali na anayesimamia nidhamu ya timu upo uwezekano mkubwa wa kumchukulia hatua kali za kinidhamu kutokana na kitendo alichokifanya.

“Pona yake ya Tshishimbi itakuwa kwa viongozi kumtetea au kumfi cha siku za ruhusa ambazo ameziomba, lakini vinginevyo, basi hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yake.”

Alipotafutwa Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli, kuzungumzia hilo, alisema: “Bado Tshishimbi hajaripoti kambini tangu alipoomba ruhusa ya siku tano arejee nyumbani kwao kwa ajili ya kukamilisha matatizo ya kifamilia.”

CHANZO: SPOTI XTRA

1 COMMENTS:

  1. Mikimtisha ataogopa kurejea kwakuwa inamngoja adhabu ni bora mambo kwa siasa au si hivo, upepo utampeleka kwa majirani kama ilivo kwa Kakolanya

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic