January 17, 2020




NA SALEH ALLY
NAJUA nawakasirisha sana watu kadhaa kuhoji kuhusiana na mambo kadhaa kwa kuwa tu naelewa Watanzania wengi hatupendi kukosolewa.

Bahati mbaya ambao hawataki kukosolewa, wameamua kujikita katika mali za umma, au mali zinazomilikiwa na wananchi ambazo zinatoa nafasi kwangu kuhoji kwa lengo la kuweka usawa, weledi na kufanya mambo yaende kwa usahihi.

Ninaowakera itabidi wabadilike kidogo ili tuweze kuwekana sawa na kujifunza mambo. Leo bado nipo katika Klabu ya Simba, nina jambo langu!

Jambo lenyewe ni kuhusiana na kiungo wa zamani wa Simba ambaye sasa ni kiungo mpya wa klabu hiyo, Shiza Kichuya.

Kichuya amejiunga tena na Simba na walisubiri kumtangaza wakati dirisha linafungwa. Amerejea nyumbani na huenda ni jambo la faraja ukilichukulia kawaida.

Kama utatulia zaidi, linafikirisha na mimi nimefikiria maswali kadhaa ambayo hakika yapo nimeshindwa kupata majibu kama mdau, kwamba ilikuwaje akasajiliwa!


Simba walionekana kabisa wanahitaji kupata mshambuliaji wa kati kwa kuwa tuliona wakati nahodha John Bocco akiwa majeruhi na Mbrazili Wilker Henrique da Silva akashindwa kucheza. Wakati huo, Simba ikaonekana imepwaya katika ushambulizi na Meddie Kagere akapungua makali.


 Wakati Simba ilipomuachia Wilker ilikuwa haina ubishi kwamba lazima wangeziba pengo hilo kwa mshambuliaji ambaye huenda angekuwa hatari zaidi kuhakikisha wanaumaliza msimu vizuri zaidi na mwisho kuingia katika michuano ya Caf.



Kilichonishangaza, siku chache zilizopita Simba walimsainisha kiungo, Luis Miquissone kutoka UD Songo ya Msumbiji ambaye unaona kwa umbo lake dogo na aina ya uchezaji na suala la nafasi, hakuna tofauti na Shiza Kichuya. Kwa nini wasajili mawinga au viungo wawili wanaofanana ndani ya dirisha moja wakati tatizo la Simba lilishaonekana kuwa ni mshambulizi?
Wakati wanamsajili Kichuya, ukiachana na Miquissone, tayari Simba walikuwa na Hassan Dilunga, Francis Kahata, Ibrahim Ajibu, Miraji Athumani, Clatous Chama na Rashid Juma wanaoweza kucheza pembeni katika namba ambayo Kichuya amesajiliwa.

Bado ninaamini Kichuya ni mchezaji mzuri lakini hakika Simba hawakuwa wanamhitaji kipindi hiki kwa maana ya nafasi anayocheza. Kama ni kweli alikuwa anahitajika na idara husika kwa maana ya benchi la ufundi, basi tukubali wakati wa usajili kulikuwa na haraka au kutokuwa na umakini kwa kuwa waliosajiliwa hawakuwa sahihi.

 Tukubali usajili wa kikosi unapaswa kusimamiwa na benchi la ufundi ndio maana nikasema nina hofu kama kweli Kocha Sven Vandenbroeck hawezi kuwa alipata muda wa kuchagua Kichuya asajiliwe na kama ni hivyo basi bado inashangaza kidogo.
Awali wakati naanza nilisema watu hawafurahishwi na kuelezwa ukweli. Najua nitakuwa ninawagusa, lakini mjue Simba ni timu ya Watanzania, hivyo rasilimali zake lazima zitumike kwa njia sahihi. Maana kama usajili wa Kichuya ndani ya msitu wa viungo wa Simba, hii inakuwani siasa, si sahihi.

Kwa kuwa Simba mmetuonyesha ni klabu inayotaka kujiendesha kiusahihi kwa kufuata weledi, jambo zuri mfanye mambo kwa usahihi badala ya kuyapeleka kisiasa.

Wakati mwingine mambo kama haya husababisha vitu ambavyo havikutarajiwa katika mwendo wa kikosi na klabu. Mfano, kama mwalimu atashindwa kumpa nafasi Kichuya, kama usajili wake lilikuwa chaguo la mtu au kundi, mwisho itaanza kulazimishwa acheze.

Au kama Kichuya ataingia na kufanya vema, mwisho nayo itaonyesha usajili waliofanya Simba ulikuwa na mambo kadhaa ya kubahatisha na si uhakika. Hivyo kulikuwa na matumizi mabaya ya fedha za Wanasimba kwa kuwa mwisho, hata ukifanya usajili iwe kwa kutoa au kukopa, Simba ndiyo inagharamia. Lazima hili nalo liwekewe heshima kwa maana ya nidhamu ya fedha na matumizi yake.

 Tuna nafasi ya kumuona Kichuya akirejea Tanzania, kwa mara nyingine Simba tena. Acha atupe somo.





11 COMMENTS:

  1. wewe shugulika na yanga ya simba waachie wanasimba wenyewe

    ReplyDelete
  2. Liverpool wana striker wangapi?Ni mfumo tu.Inategemea kocha anataka wachezaji wa aina gani Wacha kukariri .

    ReplyDelete
  3. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  4. Madaraka Seleman alienda Uarabuni akarudi akasajaliwa akafanya vizuri, Ramadhnai Lenny naye pia, Zamoyoni Mogella, Hata Pawasa alienda akarudi akapokelewa... Idd Pazi Wako wengi sana kaka ... hiyo ni Simba kaka waachie wenyewe ... k

    KINAKUUMA NINI?

    ReplyDelete
  5. Wakati Samatta = Aston Villa. @EPL
    Kichuya = Simba @Vodacom league

    Ahahaha bongo bana, bado Kichuya anasifiwa...

    ReplyDelete
  6. Nadhani kama kuna timu imefanya usajili makini dirisha dogo kwenye ligi kuu bara basi ni Simba. Imesaini wachezaji wawili vijana hasa ukizingatia John Boko si yule aliezoeleka labda ni umri pia.suala la kun'gan'gania kupiga makelele kuwa kwanini Simba imesaini kichuya ni upumbavu uliojaa unafiki ndani yake. Suali ni je kichuya ni mchezaji mb'aya? Jibu ni kwamba kichuya ni mchezaji mzuri tu tena sana. Sasa tangu lini umeona watu wakilalamikia ziada nzuri? Kama si unafiki kitu gani? Hivyo babu Niozima na Kinda kichuya upi usajili wa kuhoji? Wenzetu wazungu thamani ya mchezaji inapimwa kunako umri zaidi.

    ReplyDelete
  7. Saleh laiti kama Kichuya angesajiliwa Yanga usingekuwa unaandika unayoandika..,Mbona kuna mchezaji aliyekuwa anachezea biashara na akawafunga Biashara juzi huandiki..Katokea Misiri...na mara ya kwanza blog hii ilipoandika usajili wake mliandika kana kwamba Yanga imesajili mmisiri. Kama alikuwa hapati namba kule mpira hauwezi endelea.Kaondoka Ausens sasa kanda amenawiri..Wakati wa Omog alimgeuza Mkude mchezaji wa benchi..Poleni sana Yanga kumkosa Kichuya

    ReplyDelete
  8. Kwa hiyo unataka kusema Saleh Ally analia kumkosa Kichuya?Inawezekana kuwa kweli.Kizee Haruna alikaa kimya,wachezaji sita wa kimataifa kushindwa hata kukaa miezi 4 kimya!Tariq aliyekuwa mkaa benchi timu ya daraja la pili kimya!Anzisha timu yako .Eti timu ya watanzania!TIMU Ina Bodi nä wao na benchi la ufundi ndio wanaotoka uamuzi. Mbona gazeti la Champion unajifanya kazi liba makosa kibao hakuna anayewaingilia?WACHA unafiki wewe sio mwanachama au mpenzi wa Simba.Tuache na timu yetu.Agenda yako haiwezi kufanikiwa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic