January 17, 2020

JURGEN Klopp, Kocha Mkuu wa Liverpool amesema kuwa alimaliza mapema mgogoro wa nafsi kati ya Mohamed Salah na Sadio Mane uliotokea ndani ya timu yake mwezi Agosti,2019.
Mshambuliaji Sadio Mane alionekana kumlalamikia Salah kwa kushindwa kumpa pasi ya wazi wakati akitoka alipofanyiwa mabadiliko.
Kwenye mchezo huo dhidi ya Burney uliochezwa Uwanja wa Turf Moor, Salah aliamaua kupiga shuti badala ya kutoa pasi na timu yake ilishinda mabao 3-0.
Klopp amesema kuwa:" Kwenye mpira kuna maajabu sana unaweza kumtazama mchezaji namna anavyofanya na ukapata maneno rasmi anayoongea, niliona kama Mane amesema 'Ohh kwa nini umeamua kufanya hicho ulichofanya,? ila ni maisha ya mpira na yote lazima yatokee.
"Haikunichukua muda mrefu  baada ya mechi nilikaa nao wote na nikazungumza nao kwa muda usiopungua dakika 15, na sasa unaona wana furaha na masiha yanaendelea," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic