January 13, 2020


NAHODHA Msaidizi wa Yanga, Juma Abdul amesema kuwa kutolewa kwao kwenye hatua ya nusu fainali na Mtibwa Sugar ni matokeo ya uwanjani na wala hawajaikimbia Simba.
Abdul amerejea kwenye ubora wake kwa sasa na amekuwa mhimili kwenye safu ya ulinzi ana asisti moja kwenye ligi mpaka sasa akiwa amecheza jumla ya mechi tisa za ligi sawa na dakika 810.
Abdul amesema kuwa wachezaji walijituma mwanzo mwisho ila bahati ikawa mbaya kwao wakashindwa kulinda bao walilofunga mapema.
“Wachezaji walicheza kwa kujituma na walitimiza malengo yao ila bahati haikuwa kwetu kwani kusawazisha bao dakika za lala salama haikuwa na maana kwamba tunaiogopa Simba.
“Kwa sasa tumerejea Bongo tunajipanga kwa ajili ya mechi zetu za ligi pamoja na kombe la Shirikisho, kikubwa mashabiki watupe sapoti,” amesema Abdul.

5 COMMENTS:

  1. Kama hamumuogopi Simba, mtatayaona makucha yake wakati utapowadia

    ReplyDelete
  2. ukweli mlimkimbia Mnyama!
    sasa kwa nini baada ya kutolewa na Mtibwa mlipiga makofi kwa fujo pamoja na msemaji wenu kama siyo unafiki?

    ReplyDelete
  3. Kwa hiyo walijua kama watakutana na Simba au walipiga makofi kutokana na kupigwa dakika za mwisho?

    ReplyDelete
  4. Ni kitendo cha aibu kwa wanaoitwa mabingwa wa jadi kupiga makofi kuonesha furaha Yao kuwa wamenusurika kukutana na Mnyama jambo ambalo lingemfanya kocha wao mpya ajione mnyonge kwa kuwa yeye kwa asilimia kubwa kaletwa ili amnyanganye Mnyama ubingwa na huku Kuna kila Aina ya dalili kuwa Mnyama keshatangulia mbali na kumfikia itahitaji miujiza

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic