January 4, 2020


UONGOZI wa Klabu ya Singida United umetangaza kuingia mkataba wa miezi sita na waliokuwa wachezaji wa Yanga hivi karibuni, Haruna Moshi ‘Boban’, Haji mwinyi aliyekuwa KMKM ya Zanzibar na Tumba Lui ili kukiongezea nguvu kikosi hicho kilicho mkiani mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara msimu huu.

Singida mpaka sasa imeshakamilisha usajili wa wachezaji sita ikiwa ni katika harakati ya kukinusuru kikosi hicho kinachoonekana kuwa dhoofu msimu huu.

Msemaji wa Singida United, Cales Katemana, alisema kuwa bado wanaendelea kukiimarisha kikosi chao kuendana na mapendekezo ya kocha Ramadhan Nswanzurimo.

“Tunaendelea kufanya usajili kuendana na mapendekezo ya mwalimu na hivi leo (jana) tumekamilisha usajili wa kina Boban na wenzake ambao wamejiunga nasi kwa mkataba wa miezi sita.

“Kwa sasa tumeweka nguvu katika kusajili wachezaji wenye uzoefu kwa kuwa tunaamini kwa uzoefu walionao wataisaidia timu kufanya vizuri kwenye michezo yetu ijayo,” alisema Katemana.

Singida ambayo juzi ilipoteza mchezo dhidi ya Azam FC, ndiyo timu inayoshika mkia katika msimamo wa ligi kuu ikiwa imeshacheza michezo 13, ikishinda mmoja tu, imepoteza michezo nane na kusuluhu mechi nne.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic