January 4, 2020


KIUNGO wa Simba, Hassan Dilunga ametamba kwamba kitakachowafanya washinde mechi yao dhidi ya Yanga ni kutokana na kutaka kuwaacha mbali katika msimamo kwa ajili ya kujitengenezea mazingira mazuri ya kutetea ubingwa wao.

Timu hizo mbili zinakutana wakati Simba wakiwa kinara katika msimamo wakiwa na pointi 34 wakati Yanga wakiwa nafasi ya tatu kwa kukusanya pointi 24.

Dilunga ameeleza kuwa ni lazima washinde mechi hiyo kwa sababu ni miongoni mwa timu tatu ambazo zinagombea ubingwa, hivyo ni lazima wawafunge kwa ajili ya kujiweka sehemu salama katika msimamo wa Ligi Kuu Bara.

“Ukizungumzia juu ya timu tatu ambazo zinagombea ubingwa basi ni Simba, Yanga na Azam FC na kama unataka utwae ubingwa ni lazima uzifunge timu pinzani ambazo utacheza nazo kati ya hizo.

“Ni lazima tushinde mechi hii kwa ajili ya kutengeneza gepu kubwa la pointi. Tunajua itakuwa ngumu kufanya hivyo lakini ni lazima tufanye hivyo kwa kushinda na tutapambana kwa ajili ya kutimiza hilo,” alisema kiungo huyo.

2 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic