KIRAKA wa Simba, Erasto Nyoni amefunguka kuwa, baada ya kukamilisha mchezo wao dhidi ya Ndanda sasa mtazamo wao upo kwa watani wao, Yanga.
Simba na Yanga zinatarajiwa kukutana kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa ikiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara. Mara ya mwisho zilipokutana, Simba iliibuka na ushindi wa bao 1-0.
Nyoni alisema moja ya mipango ya Simba ni kuhakikisha wanashinda kila mchezo ulio mbele yao ukiwemo dhidi ya Yanga, hivyo wapinzani wao hao wajiandae kwa ushindani mkali.
“Baada ya kuwafunga Ndanda (Jumanne iliyopita), ndiyo tunaangalia mechi yetu inayofuata dhidi ya Yanga, tupo vizuri,” alisema Nyoni.
0 COMMENTS:
Post a Comment