MABAO ya kusawazisha ya Mapinduzi Balama na Mohammed Issa ‘Banka’, yamesababisha majonzi makubwa kwa wenzao Simba ambao wamejikuta wakikosa Sh milioni 70, kisa sare waliyoipata dhidi ya Yanga juzi Uwanja wa Taifa, Dar, wakiwa wametangulia kufunga 2-0.
Mabao ya Simba yalifungwa na Meddie Kagere na Deo Kanda wakati yale ya Yanga yalifungwa na Balama Mapinduzi na Mohammed Issa ‘Banka’. Kama Simba wangekomaa na kupata ushindi, maana yake mfungaji bora wa Wekundu, Kagere angepata Sh milioni 70 ambazo angegawana pasu kwa pasu na wachezaji wenzake wote.
Mabosi wa Simba walikuwa wameahidi kugawa kiasi hicho cha fedha kwa wachezaji wao kwenye mechi hiyo ambayo ilichezwa juzi Jumamosi katika Uwanja wa Taifa, Dar. Chanzo kutoka Simba kimelidokeza Championi Jumatatu, kuwa fedha hizo waliahidiwa wachezaji na benchi lao la ufundi endapo kama wangeshinda mechi hiyo.
“Kulikuwa na kiasi kilishatengewa kabisa cha wachezaji na benchi la ufundi kuchukua kama wangeshinda mechi ile na Yanga.
“Lakini kwa sababu walishindwa kutimiza hilo, hakuna ambaye aligawiwa fedha hizo kwa sababu tayari walikuwa hawajatimiza kile ambacho walitakiwa wakifanye,” kilisema chanzo hicho.
Akizungumzia hilo, nahodha wa Simba, John Bocco, alisema: “Kila mechi huwa kuna ahadi tunapewa na viongozi. Lakini siwezi kutaja kiasi gani tuliahidiwa kwa kuwa ni siri kati ya wachezaji na viongozi.
0 COMMENTS:
Post a Comment