January 18, 2020

ALIYEKUWA nahodha wa Manchester United, Ashley Young amekamilisha dili lake la kujiunga na klabu ya Inter Milan.
Beki huyo mwenye miaka 34 hakuwa tayari kubaki ndani ya United ambayo ilikuwa na mpango wa kumuongezea mkataba mpya amejiunga na Inter Milan kwa kandarasi ya miezi sita.
Young alijiunga na United mwaka 2011 kwa sasa amesema kuwa ni muda wake wa kuwa nje ya United kutafuta changamoto mpya.
Inter Milan inashiriki Serie A nchini Italia ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 46 baada ya kucheza mechi 19 vinara ni Juventus wana pointi 48 wamecheza mechi 19 huku United timu yake ya zamani kwenye Ligi Kuu England ipo nafasi ya tano na pointi zake 34 baada ya kucheza mechi 22.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic