BRUNO Fernandes alifungua mvua ya mabao dakika ya 42 kwa kuitungua Watford kwa mkwaju wa penalti na kuifanya Manchester United kwenda mapumziko ikiongoza kwa bao 1-0.
Kipindi cha pili United walitumia dakika tatu kufunga bao la pili kupitia kwa Anthony Martial aliyefunga bao hilo dakika ya 58.
Msumari wa tatu na wa mwisho ulikomelewa na Mason Greenwood dakika ya 75 na kuipa pointi tatu United ikiwa nyumbani Old Trafford kwa ushindi wa mabao 3-0.
Ushindi huo unaifanya United kuwa nafasi ya tano kwenye msimamo na ina pointi 41 ikiwa imecheza mechi 27 Watford ipo nafasi ya 19 na pointi 24 imecheza mechi 27.








0 COMMENTS:
Post a Comment