February 16, 2020

KIKOSI cha Yanga jana kimebanwa mbavu kwenye Uwanja wa Taifa mbele ya wajelajela Tanzania Prisons kutoka Mbeya kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara kwa kulazimisha sare ya bila kufungana.
Yanga iliyo chini ya Luc Eymael ambaye ni Kocha Mkuu walianza mpira kwa kasi kuliandama lango la Prisons ila uimara wa mlinda mlango Jeremiah Kisubi ulivuruga mipango ya washambuliaji wa Yanga wakiongozwa na Bernard Morrison.
Morrison ambaye alicheza mchezo wa jana kibabe alikwama kupeleka furaha jangwani kwani dakika ya 72 alipaisha penalti baada ya mwamuzi kutafsri kuwa amechezewa faulo na mlinda mlango Kisubi ambaye alionyeshwa kadi ya njano.
Sare hiyo iliwafanya Yanga watoke kinyonge uwanja wa Taifa wakiwa wamecheza jumla ya mechi 20 na kujiwekea kibindoni pointi 39.
Mchezo wa kwanza waliocheza Uwanja wa Samaora, Yanga iliibuka kidedea kwa kushinda bao 1-0 na ilipokutana nao kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Yanga iliwafunga mabao 2-0 ambapo Morrison alifunga bao lake la kwanza kwa mkwaju wa penalti kwa Yanga.


1 COMMENTS:

  1. Saleh Ally kiwiko cha Morisson dhidi ya Jeremiah wa Prisons mpaka akashindwa kuendelea nä mchezo ni sehemu ya mchezo mbona haizungumziwi??

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic