JOHN Bocco, nahodha wa Simba jana amekiongoza kikosi chake kuibuka na ushindi wa bao 1-0 mbele ya Lipuli kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Samora.
Bocco ambaye amerejea kwa kasi kwenye kikosi cha Simba kwa sasa akitokea kupona majeraha yake aliyokuwa anayatibu alifunga bao lake la tatu mbele ya Lipuli.
Bao pekee la Bocco lilifungwa dakika 23 kupitia shuti kali alilolipiga akiwa ndani ya 18 akimalizia pasi ya kiungo mshambuliaji Francis Kahata.
Ushindi huo unaifanya Simba kufikisha pointi 56 kibindoni ikiwa imecheza mechi 22 za ligi na imefunga jumla ya mabao 46.
Sven Vandenbroeck ameweza kuongoza kikosi chake kushinda mechi mbili mfululizo ikiwa ugenini na Bocco naye kuhusika kwenye ushindi wa mechi zote mbili.
Baada ya kupigwa na JKT Tanzania Uwanja wa Uhuru kwa kufungwa bao 1-0 hasira zao walihamishia kwa Mtibwa Sugar na Simba ilishinda mabao 3-0 na jana ilishinda bao 1-0.
0 COMMENTS:
Post a Comment