February 5, 2020


IMEELEZWA kuwa michuano mikubwa ya SportPesa Super Cup ipo njiani kurejea tena na safari hii ushindani ukitajwa kuwa mkubwa zaidi ya msimu ulipita.

Mdhamini mkuu wa michuano ya SportPesa Super Cup ni Kampuni ya kubashiri ya SportPesa ambayo imewekeza kwenye kuinua soko la mpira wa Tanzania na imedhamini timu kubwa ambazo ni pamoja na Simba, Yanga, Namungo.

Habari zinaeleza kuwa kwa sasa wadhamini hao wanasubiri kutoa tamko kuhusu uwepo wa michuano hiyo ambayo hutoa fursa kwa bingwa kucheza na timu ya Everton ya England ambayo nayo pia inadhaminiwa na kampuni hiyo.

Gormahia ni bingwa mara mbili wa kobe hilo na bingwa mtetezi ni Kariobargs Sharks aliyeshinda mbele ya Bandari kwenye fainali iliyochezwa Uwanja wa Taifa.

1 COMMENTS:

  1. Kijana tunaomba kikosi cha LIPULI,acha kudhihirisha mahaba yako kwa timu flani,kumbuka wewe ni muandishi kioo cha jamii,jamii nzima ya tanzania na nje ya nchi sasa unapoonyesha uzaifu wako unajipunguzia credibility katika jina na kazi yako.jirekebishe brother.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic