February 23, 2020




Nyota wengi wa ngumi za kulipwa wamembadika bondia Tyson Fury kuwa ndiye bora zaidi kuliko wengine wote wa uzito wa juu duniani.

Mastaa hao wamesema Anthony Joshua atakuwa wa pili kwa ubora na sasa wanataka Waingereza hao kukutana ili kumaliza ubishi.

Fury amemtwanga Deontay Wilder kwa TKO katika raundi ya saba baada ya kocha wa bondia huyo Mmarekani kulazimika kutupa taulo ulingoni.

Mastaa hao wa ngumi, michezo mingine na muziki wameshea mitandaoni wakisema hawakutegema alichokifanya Fury licha ya kwamba wamekuwa wakijua ni bondir bora.

Pamoja na kumchapa Wilder, Furry anayetokea nchini Uingereza imeonyeshwa aliongoza kwa raundi zote saba, hivyo alikuwa na nafasi ya kushinda kwa pointi pia.

Muda mwingi wa pambano hilo, Wilder aliyekuwa hajawahi kupoteza alikuwa akipokea Makonde makali na raundi ya pili aliumia sikio watangazaji wakieleza alipasuliwa ngoma ya sikio.
Furry amekuwa gumzo kubwa baada ya bambino hilo ambalo Wilder alianguka mara nne ndani ya raundi saba lakini mwamuzi alihesabu mara mbili ambazo zilikuwa sahihi.













0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic