February 6, 2020


LUC Eymael, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa Tanzania inahitaji ligi yenye ushindani ili kupata wachezaji bora watakaounda timu ya taifa imara.

Akizungumza na Saleh Jembe, Eymael amesema kuwa ameona tatizo lipo kwenye mechi nyingi ambazo anacheza pamoja na zile anazozitazama kutokuwa na ushindani mkubwa jambo ambalo linaleta upinzani kwa timu chache zenye nguvu.

"Unajua ukitaka kuwa na timu bora ya taifa ni lazima uwe na ligi imara ambayo ina ushindani kwa muda ambao nimetazama ligi ya hapa kuna matatizo ambayo yanapaswa yafanyiwe kazi, kuanzia maamuzi na namna wachezaji ambavyo watakuwa wanafanya ndani ya uwanja.

"Timu nyingi zinacheza vizuri lakini si kwa kiwango ambacho kinatakiwa ni lazima ligi iwe imara na kukiwa na ligi imara kutakuwa na timu bora ya taifa,".

2 COMMENTS:

  1. Sema kwa uhakika alichosema kocha. Acheni kuchokoza mada kimtindo. Kuna mambo mazito kocha ameyasema kwa mustakabali wa soka letu.

    ReplyDelete
  2. Inaelekea kuna tatizo kubwa la kutafsiri kinyamwezi ata makocha wote wazungu wansema kingine tunaandikiwa kingine apa kunaonyesha kuwa lugha sheeda

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic