HITIMANA Thiery, Kocha Mkuu wa Namungo FC
amesema kuwa sare ya kufungana bao 1-1 ya Azam FC mbele ya Ndanda FC inampa
hofu ya kujipanga kukabiliana na wapinzani wake.
Namungo FC itamenyana na Azam FC leo, Uwanja
wa Majaliwa ikiwa na kumbukukumbu ya kushinda mabao 2-1 mbele ya KMC.
Akizungumza na Saleh Jembe, Thiery
amesema kuwa ni ngumu kwa timu yenye uzoefu kama Azam FC kulazimisha sare
kwenye uwanja mgumu wa Nangwanda jambo ambalo linamfanya atafute mbinu za
kuizuia.
“Niliutazama mchezo wa Azam, mwanzo mwisho
walikuwa wanasukuma mashambulizi na kucheza kwa mbinu tofautitofauti, kwa namna
wanavyocheza na uzoefu walionao nitatumia nguvu nyingi kuwazuia jambo ambalo
litaongeza ugumu wa mchezo.
“Kikubwa ambacho ninakifanya kwa sasa ni
kuwaandaa wachezaji wangu kisaikolojia watambue kwamba wanakutana na timu imara
na yenye kasi muda wote wasikumbuke ushindi wao uliopita,” amesema.







0 COMMENTS:
Post a Comment