Leo Jumapili, mshambuliaji wa Aston Villa, Mbwana Samatta, anatarajiwa kusimama mbele kuwaongoza wenzake kumtibulia Kocha Jose Mourinho na timu yake ya Tottenham Hotspur.
Aston Villa watakuwa wenyeji wa mchezo huo wa Ligi Kuu England uliopangwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Villa Park ambao Tottenham wana rekodi nao nzuri tu.
Katika mechi tisa zilizopita ambazo Tottenham imecheza hapo, haijapoteza hata moja, huku ikifunga jumla ya mabao 14-1 katika mechi zote hizo.
Rekodi yao hiyo inasubiriwa kutibuliwa leo huku Samatta akipewa jukumu la kuongoza mashambulizi.
Samatta aliyejiunga na timu hiyo katika usajili wa dirisha dogo Januari, mwaka huu akitokea KRC Genk ya Ubelgiji, tayari amecheza mechi moja na kufunga bao moja.
Kwa mpira gani sifa za dunia nzima anapewa samata kuliko hata ronaldo
ReplyDelete