ANTONIO Conte, Kocha Mkuu wa timu ya Inter Milan inayoshiriki Seria A ya Italia amesema kuwa alikuwa anaitaka saini ya mshambuliaji wake Rumelu Lukaku tangu akiwa anaifundisha Chelsea msimu wa 2016-2018.
Lukaku amekuwa mwiba ndani ya kikosi cha Inter Milan ambapo alisajiliwa akitokea Manchester United, kwenye jumla ya mechi 23 alizocheza amefunga jumla ya mabao 17 akiwa na wastani wa kufunga bao moja kila baada ya dakika 116.
"Ni mshambuliaji makini na imara akiwa ndani ya Uwanja anatumia nguvu na akili nyingi jambo linalomfanya awe bora muda wote na nilikuwa ninahitaji kufanya naye kazi tangu nikiwa ndani ya Chelsea.
"Bado ni kijana mdogo na ana nguvu za kuendelea kuwa bora, matumaini yangu atafanya makubwa zaidi ya hapa kikubwa ni kuendelea kujituma na kufanya kile ambacho atakuwa anaelekezwa," amesema.
Inter Milan ipo nafasi ya kwanza kwenye Seria A ikiwa na pointi 54 baada ya kucheza mechi 23, ipo sawa na Juventus iliyo nafasi ya pili kwa pointi ila kinachowaweka nafasi ya kwanza ni idadi ya mabao.
Inter Milan imefunga jumla ya mabao 48 huku Juventus ikiwa imefunga jumla ya mabao 44.
0 COMMENTS:
Post a Comment