February 24, 2020


SIMBA imeweka rekodi yake ndani ya Ligi Kuu Bara kwa  kuwa ni timu yenye mabao mengi kuliko zote kwa sasa huku ikiwapoteza kwa mbali watani zao wa jadi Yanga.

Simba imefunga mabao 50 kwenye mechi zake 24 ambazo imecheza huku ikiongoza ligi na pointi zake 62.

Watani wao wa jadi Yanga wameachwa nyuma licha ya kuwa na mechi mbili mkononi kwani Yanga imecheza mechi 22 imefunga mabao 25 na ina pointi 41 kibindoni.

Ina deni la pointi 21 ili kuweka mzani sawa huku kwenye upande wa mabao ikidaiwa mabao 25 ili kuweka usawa na Simba yenya mabao 50.

Singida United iliyo nafasi ya 19 ndiyo inayofunga kwenye hesabu za timu zenye mabao machache imecheza mechi 24 na imefunga mabao 13 ikiwa imejikusanyia pointi12.

Kinara wa utupiaji kwa Simba ni Meddie Kagere mwenye mabao 14 na kwa Yanga ni David Molinga mwenye mabao saba.

4 COMMENTS:

  1. kuna wananchi na wenye nchi #umegundua nini?

    ReplyDelete
  2. Kama wananchi wanajulikana,basi hata wenye wanajulikana haina haja yakupepesa macho,haina tofauti na msemo wa mfuga mbwa.ha ha ha ha ha ha povu ruksaaaaa.

    ReplyDelete
  3. Wenye nchi hoyeeeeee!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  4. Nilishatambua kitamb sana na kuwambia washangiliaji na mashabiki kuwa huwezi kuwa mwananchi bila kuongozwa na wenye nchi na leo linajidhihirisha wazi kuwa kuna wananchi na wenye nchi ambao wakisema leo hakuna kwenda makazini ofisi zinafungwa hakuna wa kuhoji. duuuuuuuuuu inapenyaaaaaaaaa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic