February 23, 2020


LUC Eymael, Kocha Mkuu wa Yanga anafanya tathimini ya wachezaji wake tisa wa kigeni ambao wapo ndani ya kikosi hicho ili kujua uwezo wao.

Yanga imecheza mechi 21 ikiwa na pointi zake 40 imefunga mabao 25 na kufungwa mabao 18.

Wachezaji hao wameanza kuwekwa kwenye tathimini na Mbelgiji huyo kutokana na mwenendo wa timu ulivyo kwa sasa.

Kwenye mechi tatu za hivi karibuni Yanga ililazimisha sare na kuvuna pointi tatu na mabao mawili jambo linalompasua kichwa Eymael.

"Kwa sasa anawatazama wachezaji wa kigeni ili kujua atafanya jambo gani hasa kwenye kupanga kikosi chake kwenye mechi za ligi," kilieleza chanzo hicho.

Wachezaji wageni wa Yanga ni pamoja na :-David Molinga (Congo), Lamine Moro (Ghana), Bernard Morrison ( Ghana), Haruna Niyonzima (Rwanda), Yikpe Gnamien (Ivory Coast), Farouk Shikalo (Kenya), Patrick Sibomana (Rwanda) na Erick Kabamba (Zambia).

Eymael amesema kuwa:-"Kila mchezaji ndani ya Yanga ana kitu chake peke yake inahitaji muda kuwatambua na kuwapa nafasi ya kujua falsafa zao.

6 COMMENTS:

  1. Kila siku story ile ile,tumechoka,fukuza

    ReplyDelete
  2. Ndio ipo tamaa hapo sasa ni maongezi ya udhaifu wa wachezaji na wiki moja tu iliyopita kuwasifu jamani mabilioni yameshaangamia kukijenga kikosi na Hao watowaji Bila ya shaka wanamtaka muona matokeo na mambo ikiwa kama ilivo au kuzidi hao wahisani ndio wataendelea kuangamiza hela Yao jamani tunaumia

    ReplyDelete
  3. Endelea kufanya tathmin ya wachezaji wakati mwenzako anaendelea kukusanya alama kila kona,mwisho tutawasuasia mechi zitakazo baki mkononi baada yakuhakikisha ubingwa.yanga punguzeni mbwembwe jamani mbona mnaboronga sana,jifanyie tathmin benchi la ufundi na sio kikos wala wachezaji.

    ReplyDelete
  4. .......inter your coment,yanga leo akipona labda suluhu.mnafeli wapi watani?

    ReplyDelete
  5. Pre season kukosi kitakuwa sawa ligi ikiisha

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic