NEVERE Tegere, nyota mpya wa Azam FC amesema kuwa sababu kubwa inayomfanya awe anatupia mabao anapopata nafasi ni mazoezi ya mara akwa mara anayoyafanya akiwa peke yake.
Tegere ametupia jumla ya mabao matatu kwenye mechi zake mbili mfululizo ambapo alianza kumtungua Aishi Manula kwenye mchezo wa Ligi Kuu uliochezwa Uwanja wa Taifa na Azam FC ikapoteza kwa kufungwa mabao 3-2 kisha ngoma akafunga kwenye ushindi wa mabao 2-1 dhidi a Ruvu Shooting mabao yote mawili.
Tegere amesema kuwa amekuwa akifanya mazoezi ya kufunga mara kwa mara jambo linalompa nafasi ya kufanya vizuri kwenye mechi zake.
"Nimekuwa nikifanya mazoezi nikiwa uwanjani pamoja na wachezaji wenzangu pia hata mimi mwenyewe nikiwa peke yangu ninafanya mazoezi ya kufunga kawaida na kwa mipira ya faulo jambo linalonifanya niwe ninafunga na kwenye mechi pia," amesema.
Tigere amejiunga na Azam FC kwenye usajili wa dirisha dogo akitokea Klabu ya Platinum ya Zimbabwe.
unadishi wa ajabu sana huu,unamzungia never tigere lkn umetumia picha ya Jodi,sasa unataka kutuaminisha nin,kwenye paragraph ya pili unamuongelea never lakn aliefunga ni ngoma...hauna proof reader?
ReplyDelete