March 12, 2020


UONGOZI wa Simba umesema kuwa kichapo mbele ya Yanga kinawaumiza na wana kila sababu ya kukubali kuchapwa kutokana na makosa yao wenyewe.

Mara ya mwisho Yanga kuibamiza Simba ilikuwa ni mwaka 2016 wakati huo Kocha Mkuu alikuwa Hans Pluijm, raia wa Uholanzi.

Bao la Bernard Morrison limeibuka baada ya miaka minne kumeguka akifunga kwa adhabu ya faulo akiwa nje ya 18 na kumtungua Aishi Manula.

Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Masingisa amesema kuwa sababu kubwa ya wao kushindwa kupata ushindi mbele ya Yanga ni wachezaji wao kushindwa kujituma ndani ya Uwanja.


 "Kipigo kinaumiza na hasa ukizingatia kwamba tulijipanga kufanya vizuri, hakuna dabi nyepesi hivyo ni vigumu kupata matokeo kiwepesi, ili kushinda ni lazima wachezaji kujitoa kwa dakika 90 kupambana," amesema.

4 COMMENTS:

  1. Wachezaji wa Simba wana tabia ya kujiona wapo vizuri kuliko timu zote. Ni ukweli kwamba kwa mchezaji mmoja mmoja hakuna timu ya kuifikia Simba. Lakini mpira ni team work huwezi kushinda on paper lazima wajitume. Ndio maana kila Simba inapofungwa kunakuwa na reaction kutoka kwa wachezaji mechi inayofuata. Inabidi viongozi wa instill tabia ya kupambana kwa wachezaji. Nimeiona kwenye mechi mbili dhidi ya Kagera huko Bukoba na dhidi ya Mtibwa mechi iliyochezwa Morogoro. Angalia fighting spirit ya Atletico Madrid dhidi ya Liverpool jana.

    ReplyDelete
  2. Simba sports club players underestimated the strength of Young Africans squad.They counted chicken before the eggs were hatched.As a result they lost the tie.Poor Simba SC!

    ReplyDelete
  3. Mbona hamtoi leo matokeo ya KMC na vyura????????

    ReplyDelete
  4. The poor Simba, the wealthier Yanga Hahaaaa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic